Asas: Vijana tumieni mitandao kuyasemea mazuri ya Rais
1 October 2024, 9:57 am
Na Adelphina Kutika
Vijana wa Uvccm mkoa wa Iringa wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kuzungumza mazuri yanayofanywa serikali na serikali ya awamu ya sita.
Agizo hilo limetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Asas,wakati akifunga mafunzo ya siku saba kwa vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa yaliyofanyika katika chuo cha Vijana cha Ihemi na kuhimiza kuwa Vijana wajikite kuelezea mafanikio ya serikali na sio kupiga picha zisizofaa.
Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Aisha Mpuya, amesema vijana waliopata mafunzo hayo ni 370 kwa lengo la kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa, kuelewa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita lakini pia kujifunza matumizi bora ya mitandao.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya Mufindi Jamsini Ng’umbi amesema semina hiyo imewajenga vijana kuwa wazalendo wa kukisemea vizuri chama na taifa kwa ujumla
MWISHO