Nuru FM
Nuru FM
31 May 2025, 1:26 pm

Teknolojia hiyo itasaidia upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mazingira, ikolojia na maendeleo ya kiuchumi.
Na Joyce Buganda
Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James amepokea ugeni wa kampuni ya CC AIRWELL kutoka Austria Barani Ulaya wenye lengo la kuwekeza katika uvunaji wa maji safi kutoka angani kwa teknolojia ya kisasa katika maneo yanayokabiliwa na ukame ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akizungumza wakati akipokea ugeni huo ofisini kwake Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James amesema kampuni hiyo itafanya uwkezaji kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Iringa hivyo itasaidiakatika uvunaji ma usambazaji Zaidi ya lita milioni 260.
DC kheri amesema uwepo wa mradi huu utasaidia katika mambo mbalimbali mojawapo ni kutunza mazingira kwa kupitia uvunaji wa hewa ya ukaa.

Mmiliki na mwanzilishi wa kampuni ya CC AIRWELL, Wolfgang Rainer Fuchs, amesema Kampuni hiyo inajishughulisha na uhifadhi na urejeshwaji wa mazingira katika maeneo yanayokabiliwa na hali ya ukame ikiwemo maeneo ya jangwa kwa kuzalisha maji safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mazingira, ikolojia na maendeleo ya kiuchumi kwa kutumia teknolojia mpya ya uvunaji wa maji yaliyo katika hewa angani.
Fuchs ameeleza zaidi akisema kuwa Kampuni hiyo inatarajia kujenga mitambo yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiwa na lengo la kuzalisha maji na kuyasambaza katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa ikiwemo mbuga ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kwa upande wake Jachinda kihwelo ambae ni mzaliwa wa Iringa na Mratibu wa mradi huo amesema wamejitahidi kuwashawishi wawekezaji kuleta mradi huo Tanzania kwa sababu ya manufaa makubwa ambayo wananchi watayapata.