Nuru FM

Magari 45 yakutwa na makosa mbalimbali Iringa

9 December 2024, 11:02 am

Msimamizi Mkuu wa Takwimu za Makosa ya Usalama Barabarani Taifa, Mwanshamba Onesmo na Kamanda Allan Bukumbi wakizungumza katika Operesheni hiyo.

Na Mwandishi wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na timu maalum kutoka Kikosi cha Usalama barabarani Makao Makuu limefanya ukaguzi wa vyombo vya moto ambapo jumla ya magari 45 yamekutwa na makosa mbalimbali.

Akizungumza kwenye operesheni hiyo katika eneo la kizuizi cha magari Igumbilo Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Takwimu za Makosa ya Usalama Barabarani Taifa, Mwanshamba Onesmo amesema kuwa Oparesheni hiyo ilihusisha ukaguzi wa jumla ya magari 125.

Sauti ya Mrakibu

Kwa upande wake Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Allan Bukumbi amepiga marufuku kitendo cha baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto, kuingiza barabarani magari mabovu na madereva kutokuwa na leseni kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka.

Sauti ya Kamanda

Kamanda Bukumbi amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea na usimamizi na udhibiti wa ajali barabarani huku akiwataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona kuna matukio ya uvunjifu wa sheria za barabarani.

Sauti ya Kamanda

 Kamanda Bukumbi ameongeza kwa kusema kuwa, imezoeleka inapofika kipindi kama hiki cha mwisho wa Mwaka, wamiliki kuingiza magari mabovu barabarani lakini pia kuruhusu watu wasio na sifa kuendesha vyombo vyao kitendo ambacho ni kibaya na hakivumiliki.

“Ni marufuku kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa na kilevi, baadhi ya magari ni chakavu, nimeamuru yafanyiwe marekebisho ndipo safari iendelee, Hakuna ajali za mwisho wa mwaka Jeshi la polisi tutaendelea kutoa elimu kwa jamii mara kwa mara”, amesema Kamanda Bukumbi.

MWISHO