Nuru FM

Ubomoaji wa vibanda 331 soko la Mafinga wasitishwa

22 May 2024, 11:03 am

Mkuu wa Mkoa Iringa Peter Serukamba akizungumzia kuhusu maazimio ya kutovunjwa kwa soko la Mafinga. Picha na Hafidh Ally

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewataka wafanyabiashara kusaini mkataba hadi kufikia jumatatu ya mei 27,2024 huku wakitakiwa kuanza kulipa kiasi cha shilingi Elfu 80 kwa mwezi kwa kila kibanda makubaliano ambayo utekelezaji wake utaanza juni mosi mwaka huu.

Na Hafidh Ally

Wafanyabiashara wa soko la Mafinga wamefikia makubalino na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ya kusaini mikataba jambo lililopelekea Zoezi la kubomoa Vibanda 331 katika soko hilo kusitishwa.

Hatua hiyo imejiri Baada ya Agizo alilolitoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba akiwa kwenye baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mafinga la kumtaka Mkurugenzi kusimamia ubomoaji wa vibanda 331 katika soko la mafinga kutoka na kitendo cha wafanyabiashara wa soko hilo kushindwa kutekeleza agizo la kusaini mkataba ndani ndani ya siku 20.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa ringa

Aidha Serukamba amesema kuwa amekubaliana na wafanyabiashara kuwa kodi ya kila kibanda itakuwa shilingi 80,000/- kila mwezi na mkataba utakuwa wa miaka 14 baada ya muda huo kuisha kibanda kitabaki kuwa mali ya halmashauri.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa ringa

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mafinga wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kuwatembelea na kutatua changamoto zao huku wakiomba kuweka kiwango cha kodi ambayo wanaweza kulipa.

Sauti ya Wafanyabiashara Mafinga

Baada ya Mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa na wafanyabiashara wameridhiana; kulipa KODI YA KILA kibanda shilingi 80,000/- kila mwezi kwa mkataba wa miaka 14 na baada ya muda huo kuisha kibanda kitabaki kuwa mali ya halmashauri, katika miaka 14 ya mkataba kibanda hakitakiwi kuuzwa kwa mtu yeyote,  madeni ya nyuma ya kodi zilizokuwa zinadaiwa kabla ya mgogoro yalipwe na wafanyabiashara hao kwa halmashauri, mikataba yote kufikia jumatatu tarehe 27/5/2024 iwe imesainiwa kukiwa na namba ya nida na jina kamili la mwenye kibanda, kodi italipwa kila mwezi tarehe 1-10 na kama kodi haijalipwa italipwa na faini ya asilimia 5 ya kodi.

MWISHO