Tembo wavamia mashamba Ruaha Mbuyuni
23 March 2024, 10:56 am
Uwepo wa tembo katika kijiji cha Mtandika umetajwa kuwa kero kwani wamewasababishia hasara ya kuharibu mazao yao.
Na Adelphina Kutika.
WAKAZI wa Kijiji cha Mtandika kata ya Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wameiomba serikali kuwaondoa Tembo wanaovamia mashamba yao na kusababisha hasara lakini pia kuhatarisha maisha yao kutokana na tembo hao kupita katika makazi yao.
Wakizungumza katika mashamba hayo wananchi hao wamesema kuwa Tembo hao mara kadhaa wamekuwa wakifika majira ya usiku na kuharibu mazao hasa zao la Mahindi na kuwapelekea kushindwa kurejesha mikopo waliyokopa kwenye mashirika ya kilimo.
Aidha wameiomba viongozi wa serikali kuwa na utaratibu wa kuwatembelea katika kijiji hicho ili kubaini changamoto zinazowakabili husasani uvamizi wa tembo hao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha mtandika ADAMU ALLY MAKUNGA amesema amefanya jitihada za kuwasiliana na (TANAPA ) ili kufukuza wanyama hao lakini hakuna mabadiliko yoyote katika kijiji hicho.
MWISHO