Wananchi wa Kitelewasi hawana imani na uongozi wa Kijiji
11 May 2023, 9:48 am
Wananchi wa kijiji cha kitelewasi Kilichopo Kata ya Ilole wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wamesema hawana imani na uongozi wa serikali ya kijiji hicho kutokana na ubadhilifu wa fedha.
Wakizungumza katika mtukutano wa hadhara wanakijiji hao wameiomba serikali kuwatafutia ufumbuzi juu ya ubadhilifu walioufanya viongozi hao kwani wamewarudisha nyuma katika maendeo.
Awali akitoa taarifa ya ufuatiliaji wa shutuma za ubadhilifu huo Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji wa ubadhilifu huo SCOLASTIKA CHANG,A amesema zoezi hilo lilianza mapema mwezi march.
Nae katibu wa timu hiyo ya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya kijiji hicho JULIANO KILAVE amesema wamebaini madeni kwa baadhi ya viongozi hao wa serikali hiyo ya kijiji ambapo jumla ya pesa hizo ni zaidi ya milioni moja na laki saba.
Akijibia taarifa hiyo ya timu ya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ARUFEO MUHANGA mwenyekiti wa kijiji cha kitelewasi amesema hakuna ubadhilifu uliofanyika kufanya ubadhilifu wa pesa za wananchi wake.
MWISHO