Wodi yazinduliwa Kilolo -Wanawake kunufaika
1 March 2023, 2:24 pm
Wodi yenye thamani zaidi ya milioni 190 yajengwa Ipalamwa baada ya kuteseka muda mrefu kwa wananchi hao.
Na Joyce Buganda.
Zahanati ya Ipalamwa chini ya shirika la GLOBAL VOLUNTEER wilaya ya Kilolo imezindua wodi ya kinamama wanaotarajia kujifungua yenye thamani ya shilingi million 194 lenye uwezo wa kuwatunza kinamama 10 kwa wakati mmoja.
Akizungumza wakati wa kuzindua jengo hilo Mkurugenzi wa GLOBAL VOLUNTEER Nayman Chavala amesema jengo hilo limefadhiliwa na familia ya Peter J king kutoka nchini marekani ambapo kina mama hao watajitunza na kuwatunza watoto wao.
Aidha Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Ipalamwa Dokta Sylas Mosha amesema kinamama hao watapata mafunzo ya lishe na kuwasaidia kinamama kuwa wazazi.
Kwa upande wao wanufaika wa huduma hiyo kutoka vijiji vya Makongo, Lulindi, Ukwega,Mkalanga na Ipalamwa wamesema wanashukuru kwa kuwajengea wodi hiyo kwani vutapunguza kasiya vifo vya mama na mtoto.