Agizo,DC Iringa Upandaji wa Miti
22 February 2023, 12:54 pm
Kulingana na jiografia ya mkoa wa Iringa kupandwa Kwa miti hiyo Kando ya barabara kutachochea utunzaji wa mazingira pia itasaidia kupunguza athari za ajali hasa katika maeneo yenye milima na maporomoko.
Na Hawa Mohammed.
Serikali ya Wilaya ya Iringa imeagiza kupandwa miti maeneo ya pembezoni mwa barabara kuu zinazoingia na kutoka wilayani humo, pamoja na maeneo mbalimbali ya miji na taasisi za elimu ikiwa ni sehemu ya jitihada za utunzaji wa mazingira.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu Wa Wilaya Iringa Veronica Kessy kwa maafisa mazingira na misitu ambapo amesema kupandwa Kwa miti hiyo Kando ya barabara licha ya kuchochea utunzaji Wa mazingira pia itasaidia kupunguza athari ya ajali za magari hasa katika maeneo yenye milima na maporomoko.
Aidha Kessy amesema ni vyema kila kijiji kikatenga eneo kwa ajili ya misitu ya kutunzwa na kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya nyuki,ili waweze kujipatia kipato na kuacha kukata miti ovyo na kuharibu mazingira.