

17 March 2025, 11:30 am
Na Adelphina Kutika
Wajasiliamali Wanawake Mkoani Iringa wamehimizwa kutumia fursa zilizopo kuwekeza katika maeneo yao ili kuongeza upatikanaji wa masoko na huduma za kibiashara ili kukuza uchumi na kuzalisha vyanzo vingi vya ajira hapa nchini.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati akifungua mafunzo kwa Wajasiliamali Wanawake yaliyoandaliwa na TWCC kwa ufadhili wa TradeMark Africa katika Ukumbi wa Royal Hotel Uliopo Manispaa ya Iringa na kusema kuwa serikali inaendelea kuwajengea mazingira bora ya biashara ili kugeza fedha za kigeni na ajira.
Awali akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasmi rais wa CHEMBA ya wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Bi. Mercy Silla amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelezea wajasiliamali wanawake na vijana kutambua taratibu za kufanya biashara kwenye soko huru la Africa (AFCFTA) .
Pendo Ndumbaro ni Mwenyekiti wa CHEMBA ya wanawake Wafanyabiashara Mkoa wa Iringa (TWCC) amesema mafunzo hayo yanakwenda kuwa msaada kwa wajasiliamali wanaozalisha bishaa zenye ubora ili zikashindanishwe kwenye soko huru la Africa kutokana na kuondondolewa kwa vikwanzo .
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo Theresia Masao ambaye ni mfugaji nyuki ameiomba serikali kuondoa kodi kwa wajasiliamali wadogo wanaonza kwani zimekuwa kikwazo kuinuka kichumi
MWISHO