

11 March 2025, 12:17 pm
Na Joyce Buganda
Vijana mkoani Iringa wametakiwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo na usindikaji ikiwemo kutumia virutubisho Ili kiboresha wa mazao na bidhaa wanazozizalisha.
Mafunzo hayo yametolewa kwa siku mbili mjini Iringa kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali, Shirika la Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) na The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania
(SAGCOT).
Akizungumza na vijana hao Katika mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi, Elias Luvanda, akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, amewasisitiza Wakulima na wasindikaji wa vyakula kutambua umuhimu wa kuzingatia kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia na mbinu za kisasa kama wanavyoelezwa na Wataalam.
Hata hivyo Luvanda amekumbusha kuwa endapo Wakulima watazalishkua kitaalam na wasindikaji wakasindika vyakula vyao kwa usahihi itasaidia kuwa na jamii isiyokuwa na upungufu wa vitamini mbalimbali.
Aidha, Meneja wa program kutoka Shirika la Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN), Winfrida Mayilla amesisitiza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Wakulima na wasindikaji wanazalisha vyakula vyenye virutubisho na viwango vinavyohitajika ili jamii iweze kupata lishe bora na kupambana na utapiamlo.
Kwa upande wake Neema Kassian, ambaye ni mkulima kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, amefafanua jinsi alivyokuwa akisindika unga wa lishe bila kuzingatia kanuni sahihi huku akiahidi kuyatumia mafunzo hayo kubadilisha namna ya usindikaji wake wa unga wa lishe.
Hata hivyo mafunzo hayo pia ni sehemu ya utambulisho wa mradi mpya wa kilimo uitwao Youth Enterpreneuship for the Future Food of Africa (YEFFA), unaolenga kuimarisha kilimo cha vijana na kuwapa fursa ya kujiajiri kwa mbinu bora za kilimo na usindikaji wa mazao Vijana hawa ambao pia wameweza kujifunza kwa vitendo jinsi ya kulima mbogamboga, matunda, na mazao mengine, huku wakijengewa uwezo wa kutengeneza vyakula bora kwa kutumia virutubisho muhimu kama vile zinki na vitamini A.