Madaktari bingwa 170 watoa huduma za kibingwa kwa wananchi Iringa
1 November 2024, 10:23 am
Na Hafidh Ally na Godfrey Mengele
Jumla ya wagonjwa 170 wamepokelewa na kutibiwa katika kambi ya madaktari bingwa wa samia awamu ya pili kwenye hospitali ya wilaya ya frelimo.
Hayo yamezungumzwa wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya kheri james aliyetembelea kambi hiyo ambapo Akitoa taarifa ya juu ya ujio wa Madaktari hao Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Iringa Dk Godfrey Mtunzi amesemea kuwa kati ya wagonjwa hao watoto ni 47.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James amesema kuwa uwepo wa madaktari bingwa utasaidia wananchi kupata huduma katika maeneo yao ili kuwa na afya imara.
Aidha DC kheri amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika hospitali ya Frelimo kupata huduma za kitabibu na kitaalamu ili kujua hali ya afya zao kwa gharama nafuu.
Madaktari Bingwa hao ni daktari Bingwa wa Upasuaji, daktari Bingwa wa kinamama na Uzazi ,daktari Bingwa wa Mifupa, daktari Bingwa wa watoto, daktari Bingwa wa magonjwa ya Ndani, na daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wameanza kutoa huduma za kibingwa kwa siku 5 kuanzia tarehe 28 mwezi wa 10 hati tarehe 1 mwezi wa 11 mwaka 2024 katika Hospitali za Wilaya na za Mkoa.
MWISHO