Nuru FM

Tanesco Iringa yahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

9 October 2024, 8:52 pm

Venacy Ndialundura ambaye  alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika Mkutano wa wadau wa Tanesco. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuhamasisha wananchi kutumia  nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kama vyanzo vya nishati.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Iringa Bi. Grace Ntungi  Katika mkutano wa wateja  wa kubwa  wa mkoa Iringa pamoja na  Utoaji tuzo kwa wateja waliochangia pato katika shirika ,Uliofanyika katika ukumbi wa Royal Palm  Manispaa ya Iringa , ambapo amesema mkakati wa Tanesco  kwa sasa ni kuhamasisha  wananchi matumizi ya nishati safi.

Sauti ya Meneja

Kwa upande wake Venacy Ndialundura ambaye  alikuwa mgeni rasim ,Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewataka wateja hao kujenga mahusiano na tanesco katika utoaji huduma ,huku akiwahimiza matumizi ya nishati safi ili kuboresha mazingira .

Sauti ya Venancy

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Asas Godfrey William kama mteja  mkubwa  amesema wanalipongeza shirika la Tanesco kuwa na ushirikano wa kutosha pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa majukumu.

Sauti ya William

Aidha, mmoja wa Wateja  wakubwa waliofika kwenye Konga hilo Phina Mungai amepongeza juhudi za mheshimiwa rais kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi tofauti na kipindi cha nyuma.

Sauti ya Mteja

Hata hivyo wateja wakubwa waliotunukiwa tuzo kwa kuchangia pato katika shirika la Tanesco ni Kampuni ya Asas kuwa mshindi wa  Kwanza ,Mshindi wa Pili kiwanda cha Karatasi Mfindi na Mshindi wa tatu Saohill wa Mufindi

MWISHO