Nuru FM

Kihenzile akabidhi majiko 2000 kwa mabalozi Jimbo la Mufindi Kusini

8 October 2024, 12:09 pm

Naibu Waziri Kihenzile akigawa majiko. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Mwakiposa Kihenzile amegawa majiko 2000 kwa mabalozi wa mashina wa Chama cha mapinduzi (CCM) katika Jimbo hilo ikiwa ni katika kuendeleza jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kihenzile amegawa majiko hayo katika mkutano maalumu wa mabalozi wa mashina Jimbo la Mufindi Kusini uliofanyika katika kata ya Igowole iliyopo Wilaya Mufindi Mkoa wa Iringa.

Sauti ya Waziri

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya ORYX Energies Tanzania Bara, Alex Wambi aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni hiyo katika Mkutano Maalum wa Mabalozi wa Mashina Jimbo la Mufindi Kusini amesema kampuni hiyo inaendelea na juhudi za kumuunga mkono raisi wa Tanzania katika harakati za kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi.

Sauti ya Afisa Masoko

Akizungumza katika mkutano huo,Naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi(CCM) Tanzania  Bara John Mongella amepongeza Kihenzile kwa kazi kubwa anayofanya serikalini na wakati huo huo akishughulikia changamoto za watu wake katika jimbo lake.

Sauti ya Mongela

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yasin Amewataka viongozi wa CCM na wanachama wake jimboni humo kuimarisha mshikamano na kuhakikisha wanafanikisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama inayoendelea kufanywa kwa ufanisi.

Sauti ya Yassin

Nao baadhi ya mabalozi wa walihudhuria mkutano huo wametoa shukrani zao kwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwaletea maendeleo katika jimbo la mufindi kusini.

Sauti ya Mabalozi

MWISHO