Nuru FM

Mbunge Kiswaga achangia milioni 1 ukarabati shule ya msingi Kidamali

3 October 2024, 6:56 pm

Mgeni rasmi katika mahafali ya 22 ya darasa la saba shule ya Msingi Kidamali Ndugu Elia Kitomo akimwakilisha Mbunge Jackson Kiswaga. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh. Jackson Kiswaga amechangia shililingi Milioni 1 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa shule ya Msingi Kidamali iliyopo Kata ya Nzihi Mkoani Iringa.

Akizungumza katika mahafali ya 22 ya darasa la saba ya shule ya Msingi Kidamali Mgeniu Rasmi Ndugu Elia Kitomo aliyemwakilisha Mh. Kiswaga amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kurekebisha  madarasa ya shule ambayo ni chakavu huku yeye mwenyewe akitoa shilingi Laki Moja.

“Niko hapa Kumwakilisha Mh. Kiswaga na amenipa salamu zake na ameniambia niwakabidhi shilingi milioni moja kwa ajili ya ukarabati wa madarasa, hivyo na mimi kwa umuhimu wa jambo hili nitachangia hapa shilingi laki moja ili kuunga juhudi za kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais Samia suluhu Hassan” Alisema Kitomo

Sauti ya Kitomo

Hatua hiyo imejiri baada ya Ndugu Kitomo kusomewa Risala ya mahafali hiyo iliyosomwa na wahitimu wa darasa la saba wa shule ya Msingi Kidamali ambapo moja ya changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni pamoja uchakavu wa majengo na upungufu wa Madawati na walimu.

Sauti ya Mwanafunzi

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Msingi Kidamali Mwl. Stanslous Nyembeke amesema kuwa mwaka jana kulikuwa na uhaba wa madawati 150 ambapo Mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga aliwaahidi kuwaandalia madawati 30 na yatafika muda wowote kuanzia sasa.

“baada ya kupewa ahadi na Mbunge kiswaga ya kuletewa madawati, kwa sasa tuja uhitaji wa madawati 120 ambapo tuna imani yakipatikana yatasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki” Alisema Mwl. Nyembeke.

Sauti ya Mwalimu Mkuu

MWISHO