Nuru FM

Wananchi Kidamali walia na kero ya barabara

11 March 2025, 8:50 pm

Wananchi wakizungumzia kero ya barabara. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Wananchi wa kijiji cha Kidamali kilichopo kata ya Nzihi Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoani Iringa wamelalamikia kero ya miundombinu ya barabara hasa kwenye kipindi hiki cha mvua za masika kuleta madhara ikiwamo kushindwa kusafirisha mazao kuletakatika masoko ya mjini.

Wananchi hao wameomba kukamilishwa kwa ujenzi wa barabara kwani pamoja na changamoto hiyo wamekuwa wakitumia usafiri wa bajaji ambao ni ghalama tofauti na awali usafiri uliokuwa msaada kwao ni daladala.

Sauti ya Wananchi

Wananchi hao wamesema ujenzi wa barabara hiyo umetolewa ahadi za viongozi wao diwani na mbunge kipindi cha kampeni lakini hakuna utekelezaji wowote.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake Diwani wa kata ya nzihi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Msembe inayoelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (km 104) kwa kiwango cha lami utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 142.56 na wakandarasi tayari wapo site pia TARURA wameanza kupita kwenye maeneo ya makazi ili kupima barabara hizo kwa ajili ya matengenezo.

Sauti ya Mhapa

MWISHO