Tuna Finance Hub kutoka UoI kuwanufaisha vijana
20 January 2025, 12:13 pm
Na Joyce Buganda
Umoja wa Tuna Finance Hub kutoka Chuo Kikuu cha Iringa wamejidhatiti kuhakikisha vijana wa Iringa wanakombolewa kiakili na kifikra katika utafutaji na jinsi ya kupata maendeleo katika sekta mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo katika chuo kikuu Cha Iringa mmoja wa waanzilishi wa Tuna finance hub Helman Minazi amesema lengo lao ni kutoa elimu ya fedha hasa kwa wanafunzi na kawafanya vijana kuwa wepesi katika kuziona fursa za kimaendeleo.
Aidha Mhadhiri kutoka chuo kikuu Cha Iringa Bi Teresia Josephat amesema wao kama chuo wanashirikiana vyema na Tuna finance hub kwa sababu katika masomo yaliyotolewa chuoni hapo ni pamoja na jinsi ya kutunza fedha katika mifuko mbalimbali ya uwekezaji, wajibu wa kifedha na uchumi katika jamii.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wamesema wanaishukuru Tuna finance hub kwa kuwapa elimu ya fedha kwani wengi wao walikuwa wanapata fedha na kutumia vibaya.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani Iringa.