Mafinga Mji yafanya ufuatiliaji wa wanafunzi waliopangiwa shule mwaka 2025
17 January 2025, 12:14 pm
Na Sima Bingilek
Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani Iringa imefanya Ufuatiliaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika Shule zetu za Sekondari tangu kufunguliwa kwa shule Jan 13 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Ufuatiliaji huo Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga Mwalimu Stephen Shemdoe amesema kuwa wamefanya ufuatiliaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti Shule walizopangiwa sambamba na hali ya utoaji wa chakula kwa wanafunzi na kuona mwitikio wa wazazi katika kuchangia chakula.
“ Tunafanya Ufuatiliaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika Shule zetu za Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga lazima tujue wanafunzi walipangiwa wangapi na wameripoti wanafunzi wangapi tangu shule kufunguliwa tarehe 13 Januari 2025 mpaka leo tarehe 16 Januari 2025 na kujua sababu inayofanya wengine wasiripoti kuanza masomo. Pia katika ufuatiliaji tunaangalia hali ya utoaji wa chakula kwa wanafunzi na kuona mwitikio wa wazazi katika kuchangia chakula “- Afisa Elimu Sekondari Mji Mafinga,Mwalimu Stephen Shemdoe.
Katikati Ufuatiliiaji huo Afisa Elimu ameweza kuzungumza na wazazi wanaowachelewesha wanafunzi kuripoti shuleni na kuwaambia umuhimu wa kuwahi shuleni pia kukagua stoo za chakula ili kuona kiwango kinachochangiwa na wazazi na kuhamasisha wazazi wasiochangia kuchangia
Akiwa katika ufuatiliaji huo, Afisa Elimu ameweza kuzungumza na wazazi wa wanafunzi wa kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari JJ Mungai na kuwataka kushirikiana na wazazi ili kuleta matokeo mazuri ya wanafunzi
Katika Shule ya Sekondari Changarawe wanafunzi waliopokelewa wa kidato cha kwanza ni 134 ambapo wanafunzi wa kike ni 66 na wanafunzi wa kiume ni 68, Shule ya Sekondari JJ MUNGAI wanafunzi waliopokelewa ni 97. Wanafunzi wa kike 31 na wanafunzi wa kiume 33 jumla 64. Shule ya Sekondari Nyamalala. Jumla ya wanafunzi 109 wamepokelewa wavulana 53 wasichana
Aidha katika ufuatiliaji huo Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Stephen Shemdoe amekagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondarii Nyamalala inayojengwa kwa mapato ya ndani na ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari JJ Mungai.