Nuru FM

Msigwa amuunga mkono Lissu uchaguzi Chadema

16 January 2025, 5:05 pm

Mwanachama wa CCM Peter Msigwa akiwa na Mtangazaji wa Nuru FM Azory Orema katika mahojiano na Nuru Digital. Picha na Ayoub Sanga

Joto la Uchaguzi wa Chadema limezidi kupanda baada ya Aliyekuwa mwanachama wa Chadema ambaye kwa sasa ni Kada wa CCM Peter Msigwa kuonesha nia ya kutamani Lissu awe mwenyekiti wa Chama hicho.

Na Hafidh Ally

Mwanasiasa mkongwe na Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Mch. Peter Msigwa, ameweka wazi msimamo wake kuhusu uchaguzi wa viongozi ndani ya chama hicho, akisema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA badala ya Freeman Mbowe.

Akizungumza na Nuru Fm Msigwa amesema kuwa anatamani Lisu awe mwenyekiti wa Chadema ili kuwafanya chama cha CCM na viongozi wake kujishughulisha kwa kuwa amekuwa ni kiongozi mwenye kujenga hoja.

Sauti ya Msigwa

Kwa upande wake Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lisu amesema kuwa ataboresha mfumo wa uendeshaji wa chama hasa katika utafutaji na usimamizi na ugawaji wa mapato ya Chama.

Sauti ya Lissu

Naye Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mboye anayewania tena nafasi hiyo amesema kuwa kuchukua lawama kutoka kwa wanachama ni sehemu ya uongozi ndio maana anapigania maridhiano katika chama.

Sauti ya Mbowe

Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kinaendelea na uchaguzi ndani ya chama hicho ambapo kimeanza na uchaguzi wa baraza la vijana Bavicha huku januari 21 kikitarajia kumchagua mwenyekiti taifa na viongozi wengine wa chama hicho.