Mafinga Mji yahakiki vikundi 62 ili vipewe Mikopo
14 January 2025, 10:17 am
Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa inatekeleza programu ya utoaji mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama ilivyo kwa Halmashauri zote nchini kutokana na Mapato ya ndani.
Na Joyce Buganda
Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa Imefanikiwa kuhakiki vikundi 62 ili kupatiwa mikopo ya asilimia 10 vikiwemo vikundi vya watu wenye ulemavu, vijana na wanawake.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji Bi. Fiderica Myovela na kuongeza kuwa vikundi hivyo vitapatiwa jumla ya shilingi Milioni mia 8 ili kutekeleza shughuli za kiuchumi.
Akizungumzia hali ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amezitaka Halmashauri kukamilisha miradi hiyo haraka iwezekanavyo ili kuongeza huduma za kijamii kwa Wananchi.
MWISHO