Nuru FM

Wananchi Iringa waaswa kuacha tabia ya kufungulia maji taka

12 January 2025, 10:57 am

Picha ya Mnara wa saa unaowakilisha nembo ya Mkoa wa Iringa.

Na Zahara Said na Halima Abdallah

Ikiwa tupo katika msimu wa mvua, wananchi Manispaa ya Iringa wametakiwa kuchukua tahadhari ikiwemo kuacha kufungulia maji taka ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko hasa kipindu pindu.

Wakizungumza  na kituo hiki baadhi ya wananchi manispaa ya  iringa wameeleza  watahakikisha wanazingatia suala la kufanya usafi pamoja na kuhifadhi taka maeneo husika ili kuepuka  magonjwa hayo.

Kwa upande wake Mratibu wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko Mkoa wa Iringa John Mwakabungu amewatoa hofu wananchi kuwa hali ya usalama mkoa wa iringa ipo shwari huku akiwataka kuwa makini kwa kuchukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa magonjwa. 

Mwakabungu ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kuachilia chemba za maji taka kwenye mitaro katika kipindi hiki kuwa ni kosa kisheria na adhabu kali zitachukuliwa kwa atakae bainika kutenda kosa hilo.

MWISHO