Nuru FM

Milion 150 zatumika kujenga ghala la dawa hospitali ya Frelimo Iringa

26 November 2024, 1:00 pm

Picha ya Muonekano wa ghala la kuhifadhia dawa katika Hospital ya Wilaya ya Frelimo Manispaa ya Iringa. Picha na Adelphina

Na Adelphina Kutika

Zaidi ya shilingi milioni 150 zimetumika kujenga Ghala la Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Frelimo, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Hayo Yamebainishwa na Mfamasia wa Hospitali hiyo, Sued Deogratius katika ziara ya mwendelezo wa Jukwaa la Mafanikio, ambapo ameeleza kuwa kupitia fedha za maendeleo ya miradi, hospitali hiyo ilipokea shilingi milioni 154 kwa ajili ya ujenzi wa Ghala hilo, ambalo litasaidia kuhifadhia dawa na vifaa tiba muhimu.

Sauti ya Mfamasia

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James, akizungumza Katika ziara hiyo amesema kuwa ujenzi wa Ghala hilo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya, hasa kwa kuhakikisha kuwa dawa na vifaa tiba vinahifadhiwa vizuri ili kusaidia wananchi katika kupata huduma bora za afya.

Sauti ya DC

Kwa upande wao, baadhi ya wazee wa kimila wamesema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanya kazi nzuri katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikumbana na changamoto za upungufu wa vifaa tiba na dawa.

Sauti ya Wazee

Hata hivyo ujenzi wa Ghala la Dawa katika Hospitali ya Frelimo ni ishara ya maendeleo katika sekta ya afya, na ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Iringa.

MWISHO