Nuru FM

Mila na desturi chanzo cha wanaume kushindwa kuripoti matukio ya ukatili

20 November 2024, 7:00 pm

Wananchi Mkoani Iringa wamesema kuwa mila na desturi katika jamii imetajwa kuwa sababu inayopelekea wanaume wengi wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kushindwa kuripoti pindi wanafanyiwa vitendo hivyo.

Wakizungumza katika kongamano la wanaume lililofanyika mkoani Iringa baadhi ya wananchi wameeleza kuwa mila na desturi za jamii nyingi zinawanyima wanaume fursa ya kuzungumza kuhusu ukatili wa kijinsia wanaokutana nao, hasa wanapokuwa wahanga wa vitendo vya ukatili kutoka kwa wake zao.

Sauti ya wananchi

Naye Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa bado wanawake ndio wahanga wa matukio ya ukatiki kwani kwa mwaka 2023/2024 wanawake wapatao 516 wamekumbwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Iringa pekee.

Sauti ya Gwajima

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, amewataka wanaume kuzingatia na kuchukua hatua stahiki ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani ushiriki wao wanaume kutasaidia kupunguza ukatili na kulinda familia.

Sauti ya Serukamba

Nao baadhi ya Viongozi wa dini waliohudhuria kongamano Hilo akiwemo Padre Steven Mvili na Shekhe Abubakari Chalamila wamewakumbusha wanaume kutimiza majukumu yao katika familia kwa kuzingatia maadili mema na kuepuka mifumo ya maisha ya sasa inayoweza kuathiri uhusiano wa familia.

Sauti ya viongozi

Hata hivyo Kongamano hilo limelenga kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa wanaume kushiriki katika kupinga ukatili wa kijinsia, likiambatana na kauli mbiu isemayo: “Wanaume, Viongozi wa Mabadiliko Chanya, Pinga Ukatili, Ondoa Msongo wa Mawazo.”

MWISHO