Nuru FM

Wanasiasa Iringa wamlilia Katibu wa CCM aliyeuliwa na wasiojulikana

14 November 2024, 9:31 am

Viongozi wa Chadema na CCM mkoa wa Iringa wakiwa nyumbani kwa marehemu Christina aliyeuawa kwa kupigwa Risasi. Picha Ayoub Sanga

Na Shaffih Kiduka

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa pole na kulaani vikali mauaji ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Bi. Christina Kibiki (56) ambaye ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Akizungumza mara baada ya kufika Nyumbani kwa Marehemu kutoa salamu za Pole, Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Iringa Mjini Frank Nyalusi amesema hali hii haijazoeleka hapa nchini na wananchi wanapaswa kuishi kwa amani na si kutendeana mabaya.

Sauti ya Nyalusi

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Iringa (MNEC) Salim Abri Asas amesema kuwa wa mepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hiyo na wanaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake kuwabaini wahusika waliotenda unyama huo.

Sauti ya Asas

Kwa upande wake mwenyekiti nwa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin amewataka wananchi Mkoani Iringa kuwa watulivu kipindi hiki ambapo jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini wahusika wa tukio hili.

Sauti ya Daud

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Marehemu alishambuliwa kwa kupigwa risasi kifuani pamoja na kupigwa na kitu kizito kichwani na Watu Wasiofahamika.

MWISHO