Nuru FM

Waziri Lukuvi aishukuru serikali barabara ya Msembe-Iringa Mjini

21 October 2024, 10:26 am

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akizungumzia kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Msembe – Iringa Mjini. Picha na Van Kahise

Na Van Kahise

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani ameishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kijiji cha Msembe lango la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mpaka Iringa Mjini.

Waziri ametoa shukrani hizo wakati wa ziara yake katika kata ya Idodi ya kutembelea miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Ujenzi wa barabara hiyo ni shauku ya watu wa Jimbo la Isimani waliyokuwa nayo kwa muda mrefu na kampuni ya Chicco ndio imeshinda tenda ya ujenzi wa kipande hicho cha barabara.

Sauti ya Lukuvi

Waziri Lukuvi amesema kuwa kwa ujenzi wa barabara hiyo itapelekea wakazi watakaopitiwa na mradi huo kupata ajira na zoezi hilo litaenda sambamba na  kuwekwa taa za barabarani katika miji ya Tungamalenga, Idodi, na Mapogoro.

Sauti ya Lukuvi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Idodi Mh. Julius Mbuta amesema anaishukuru serikali kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika kata ya Idodi, na kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama.

Sauti ya Diwani

MWISHO