Nuru FM

Uwanja Wa Ndege Wa Nduli Kuwa Lango La Fursa Ya Utalii

13 August 2022, 7:41 am

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa utakapokamilika utaongeza fursa za kibiashara na kuifungua zaidi kanda ya Kusini kwenye sekta ya Utalii.

 

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo mkoani Iringa alipokuwa akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli na akitoa rai kwa wananchi wajipange katika kuchangamkia fursa zitakazoletwa na uwanja huo katika sekta ya Utalii.

 

Rais Samia amesema uwanja hadi kukamilika ndege zenye uwezo wa kubeba hadi abiria 70 zitaweza kutua katika uwanja huo.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili ja Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana licha ya kupongeza jitihada hizo za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan za kuendelea kufungua milango ya Utalii nchini amesema uwanja huo utaongeza idadi ya Watalii kwenye vivutio vya Kanda ya Kusini, kuongeza hamasa kwa wawekezaji na chachu katika biashara ya mazao ya misitu pamoja na usafirishaji wa vyakula kwenye mikoa mingine yenye Idadi kubwa ya Watalii.

 

Naye Diwani kata ya Nduli Ndugu Bashir Mtove amesema uwanja huo utafungua fursa ya kibishara na utalii huku akiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa kituo cha polisi na na barabara itakayo chepuka kupitia kigonzile ili makubwa ya miziigo yaweze kutumia barabara hiyo kuepusha msongamano wa katika barabara kuu ya Dodoma.

Nao Baadhi  ya Wananchi wa mtaa wa mapanda kata ya Nduli Manispaa ya Iringa wameeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege na kuruhusiwa kutua ndege kubwa kutasaidia kukuza uchumi wa mkoa na wawananchi kwa ujumla.

 

Uwanja huo unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi Augosti 2023 utagharimu Bilioni 63 ambazo ni pesa za ndani na mkopo kutoka benki ya Dunia.