

14 March 2025, 12:11 pm
Na Adelphina Kutika
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limewapongeza wakaguzi na askari waliofanya vizuri mwaka 2024 ili kuongeza chachu kwa wengine kufanya kazi kwa nidhamu na weledi
Akizumgumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vyeti hivyo kamanda wa polisi mkoa wa iringa ACP Allan Bukumbi katika viwanja vya FFU Kihesa amesema lengo la kutoa motisha na kuthamini utendaji kazi kwa askari hao na kuongeza morali katika utekelzaji wa majukumu.
Awali akiawasilisha taarifa fupi mbele ya Mgeni Rasim mkuu wa kitengo operation na Mafunzo mkoa wa Iringa meloy Buzema amesema hafla hiyo ya kutambua utendaji kazi kama mkoa wameona achache waliofanya kazi vizuri wakaguzi 2 na askari 6.
Kwa upande wao waliotunukiwa vyeti vya sifa ya pongezi akiwemo Mkaguzi Msaidizi kata kata ya Mkwawa Feruzi Makamba amepongeza uongozi wa jeshi la polisi kwa kutambua mchango wao na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kwa weledi.
Hata hivyo huo ni utaratibu wa wa kawaida kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kutambua na kutambua na kuwa pongeza askarin na wakaguzi waliofanya vizuri ili kuhamasisha utndaji kazi kujenga taswira chanya ka jamii.
MWISHO