CHADEMA Iringa wasusia uchaguzi Serikali za mitaa
27 November 2024, 12:15 pm
Na Azory Orema
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Iringa Mjini kimesusia uchaguzi wa serikali za mtaa kwa kilee walichokiita kutoridhishwa na mwenendo mzima wa msimamizi wa uchaguzi jimbo la iringa mjini.
Akizungumza na Nuru Fm mwenyekiti wa Chama Cha Dermokrasia Na Mandeleo {Chadema} Jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi amesema kuwa wameamua kuchukua mamuzi hayo kutokana na kutotendwa haki kwa mawakla wa chama hicho kwa kutopokelewa na wengine kunyimwa vibali.
Pamoja na juhudi za msimamizi wa uchaguzi kuruhusu mawakala kusimamia zoezi hilo baada ya majadiliano nyalusi ametaja sababu za mawakala wao kutopigiwa muhuli.
Awali mkuu wa mkoa wa iringa akiwa katika kituo chake cha kupigia kura amesema waliamuru kusitisha kwa muda mchache zoezi la upigaji kura ilin mawakala wa chadema wagongewe mihuri kwenye fomu zao ili vyama vyote vishiriki uchaguzi.
Itakumbukwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliagiza uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike pasipo vurugu kwa kulinda amani tulionayo huku akitaka wapiga kura waheshimiwe ili kutimiza wajibu wao.
MWISHO