Nuru FM

DAS Kyando: Tunzeni Miundombinu ya Umeme

1 November 2024, 10:36 am

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Stomen Kyando akikata utepe kiashiria kuzinduliwa kwa Miundombinu ya Umeme. Picha na Ayoub Sanga

Na Adelphina Kutika

Wananchi wa Kitongoji cha Itemela na Mpilipili, kata ya Nyazwa, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, wamehimizwa kutunza miundombinu ya umeme iliyozinduliwa katika kijiji chao.

Akizungumza baada ya hafla ya uzinduzi wa umeme na utoaji elimu, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Iringa, Mhandisi Grace Ntungi, amesema mradi huu umegharimu milioni 144 za Kitanzania, na akasisitiza umuhimu wa utunzaji wa miundombinu hiyo.

Sauti ya Mhandisi

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya kilolo ,Katibu tawala STOMEN KYANDO  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo  amewataka wananchi wa vijiji hivyo watumie fursa ya kuweka umeme  kwa bei  iliyopo kwa sasa kabla miongozo na sera hazijibadilika

Sauti ya DAS

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Nyazwa BONIPHASI NGWALE ame   toa ombi kwa Tanesco, akitaka kuwepo kwa uboreshaji wa miundombinu ya umeme ili kuongeza fursa za kimaendeleo katika kijiji cha Nyazwa.

Sauti ya Diwani

Hata hivyo Hii ni fursa muhimu kwa wananchi wa Nyazwa, na ni muhimu kwa kila mmoja kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuleta maendeleo endelevu.

MWISHO