Chifu wa wahehe aongoza wazee wa kabila hilo kufanya utalii hifadhi ya Ruaha
2 October 2024, 10:25 am
Na joyce Buganda
Chifu wa Kabila la Wahehe Mkoani Iringa Adam Abdul Mkwawa ameongoza kundi la wazee kwenda kufanya utalii wa ndani katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikiwa ni ufunguzi wa kusherehekea Miaka 60 toka hifadhi ya Taifa ya Ruaha ilipoanza.
Akizungumza akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Chifu Adam Abdul Mkwawa ambae ndiyo kiongozi wa kabila la wahehe amesema kutembelea hifadhi hiyo ni moja ya kumuenzi Mkwawa mwenyewe kwani Kuna historia yake.
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Godwell Meing’ataki amesema kundi la wazee limeanza na makundi mengine kama viongozi wa dini na watu wenye ulemavu yatafuata kwenda kutalii hifadhini Ruaha hiyo yote ni shamra shamra za kusherehekea Miaka 60 ya hifadhi ya Ruaha pamoja na kutangaza utalii wa vivutio vilivyomo ikiwa ni pamoja na kuvilinda.
Hata hivyo baadhi ya wazee wa kimila wamesema wamefurahi kutalii kwenye hifadhi hiyo ya Ruaha na wameahidi kuendelea kudumisha Mila alizoziacha Mtwa Mkwawa huku akiwasistiza wananchi kuacha ujangili na kuacha kukata miti ovyo.
Kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi ya taifa ya Ruaha yatafanyika tarehe 7 mwezi wa 10 hifadhini Ruaha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa maliasili na utalii Mh. Pindi Chana.
MWISHO