Nuru FM

Kada wa Chadema Iringa mbaroni kwa ulevi na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni

2 October 2024, 10:02 am

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akizungumzia kukamatwa kwa Nkuna. Picha Na Ayoub Sanga

Na Ayoub Sanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limemkamata Vitus Nkuna (29) Mjasiriamali, Mkazi wa Mwangata Manispaa na Mkoa wa Iringa kwa kosa kusababisha ajali barababarani akiwa amelewa na kuchapisha taarifa za uongo Mtandaoni.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Mtuhumiwa huyo alisababisha ajali eneo la Mgongo kata ya Nduli na kukimbia.

“Nikwamba, Septemba 30, 2024 eneo la Mgongo kata ya Nduli barabara ya Iringa Dodoma. ndugu Nkuna akiendesha gari aina ya Volkswagen touareg rangi nyeusi yenye namba za usajili T 797 DYC alisababisha ajali kwa kuligonga gari aina ya Toyota Probox rangi nyeupe yenye namba za usajili T 975 EDC mali ya Kampuni ya KINGS inayojishughulisha na usambazaji wa pombe kali ikiendeshwa na ndugu Goodliving Moshi (35) Mchaga. mfanyabiashara, mkazi wa Mkimbizi na kisha kukimbia”

Sauti ya Kamanda

Amesema kuwa Mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na kiwango kikubwa cha pombe ambapo baadaye lichapisha taarifa kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter) kuwa ameshambuliwa na Watu wasiojulikana akiwa barabarani Mkoani Iringa baada ya mapambano na kupelekwa kituo cha Polisi Iringa.

Sauti ya Kamanda

Sambamba na hilo Bukumbi amesema kuwa Mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo  Mtandaoni na kosa la ulevi akiwa anaendesha gari na baadaye atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.

Sauti ya Kamanda

MWISHO