Nuru FM

Bilioni 1.6 kujenga shule ya elimu ya amali Mafinga Mji

26 September 2024, 9:45 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mafinga Mji. Picha na Ayoub Sanga

Na Hafidh Ally

Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Umma inayotoa elimu ya Amali (Ufundi) katika kata ya Changarawe Halmashauri ya Mafinga Mji mkoani Iringa.

Hayo yamezungumzwa na  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Miradi  Mjini Mafinga ambapo amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kutatua tatizo la ujinga nchini kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye Elimu.

Sauti ya Serukamba

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa amebainisha kuwa watahakikisha wanasima utekelezaji wa Miradi hiyo kabla ya tarehe 31 mwezi wa kumi iwe imekamilika.

Sauti ya Linda

Naye Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mafinga Maji Bi. Fidelika Myovela amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwapatia zaidi ya Bilion 3.35 kwa ajili ya shule za sekondari jambo ambalo litasaidia kukuza sekta ya elimu.

Sauti ya Fidelika

Akizungumzia utekelezaji wa Miradi hiyo, Mhandisi wa halmashauri ya Mafinga Mji Bw. Christopher Nyamvugwa  amebainisha kuwa wamekuwa wakipata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa halmashauri hiyo jambo linalopekelekea miradi ikamilike kwa wakati.

Sauti ya Mhandisi

MWISHO