Nuru FM

DC Kheri: Lindeni rasilimali za chuo cha VETA Pawaga

26 September 2024, 9:49 am

Mwonekano wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichopo Pawaga Wilaya ya Iringa. Picha na Joyce Buganda.

Na Joyce Buganda

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James amewasihi wananchi Wilayani Iringa kuhakikisha wanalinda rasilimali zilizowekwa katika chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichopo Pawaga wilaya ya iringa.

Kheri James ameyasema wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya chuo hicho na kuwataka wananchi hao wawathamini watumishi na kuhahidi kuwa serikali itazishughulikia changamoto zilizopo.

Sauti ya DC

Aidha amesema lengo la serikali kuanzisha chuo hicho ni kuongeza wigo wa vijana kujiajiri kwa kupata ujuzi tofauti tofauti.

Sauti ya DC

Awali Mkuu wa chuo hicho Petronia Shata akiwasilisha taarifa ya chuo kwa mkuu wa wilaya ameeleza changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho ikiwa ni pamoja na kukosa gari la gari la kufundishia udereva kwa mafunzo ya vitendo na uhaba wa Watumishi wa kufundisha.

Sauti ya Mkuu wa chuo

MWISHO