Nuru FM

DC Kheri: Viongozi wa dini shirikianeni na waumini katika uzalishaji

16 September 2024, 1:22 pm

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Kheri James akizungumza kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa dini. Picha na Joyce Buganda.

Viongozi wa dini wametajwa kuwa msaada katika kuhakikisha wananchi wanashiriki katika Shughuli za kijamii.

Na Joyce Buganda

Viongozi wa dini Wilaya ya Iringa wametakiwa kuwajibika na kuwahimiza waumini wao wanashiriki katika shuhuli za maendeleo hasa za uzalishaji mali.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James wakati akizungumza na viongozi wa dini wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika kikao na viongozi hao na kuongeza kuwa viongozi wa dini wakishirikiana na wananchi itaongeza uwajibikaji na maendeleo.

Sauti ya DC Kheri

DC kheri amesema kila mtumishi akiwajibika vizuri kwa kushirikiana na Viongozi wa dini, kutakuwa na huduma bora za kijamii zitaimarika.

Sauti ya DC Kheri

Hata hivyo DC KHERI amesema  viongozi wa dini  wanatakiwa kuungana na serikali katika kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo.

MWISHO