Nuru FM

Jaji Mbarouk: Jitokezeni kuboresha taarifa katika daftari la mpiga kura

16 December 2024, 12:54 pm

Viongozi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika picha ya Pamoja na wahariri ambao ni wadau wa uchaguzi. Picha na Ayoub Sanga

Na Hafidh Ally

Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imewataka wananchi Mkoani Iringa kutojiandikisha zaidi ya mara moja katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajia kuanza Dec 27 mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa Tume na Wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Makamu Mwenyekiti Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Jaji Mbarouk S. Mbarouk amesisitiza kuwa ni kosa kisheria mtu mmoja kujiandikisha jina lake la kupiga kura zaidi ya mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Sauti ya Jaji Mbarouk

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa mahakama na Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Asina Omary amewashukuru wadau wa uchaguzi kwa kushiriki katika mkutano huo huku Tume ikiahidi kupokea maoni na kuyaboresha kwa maslahi ya uchaguzi.

Sauti ya Asina

Awali Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Kheri james amesema kuwa wanatarajia kupitia wadau hao wananchi wote wenye sifa watajiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la Maboresho la Mpiga kura.

Sauti ya DC

Makundi yanayotakiwa kwenda kufanya uboreshaji wa taarifa zao,ni wale watakao timiza umri wa miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi Mkuu  2025 ,wale waliojiandikisha awali na kuhama Kata au Jimbo kwenda maeneo mengine, wale wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji hapo awali na wale waliopoteza kadi zao ya kupiga kura au wenye kadi zilizoharibika.

MWISHO