Wafugaji Iringa waaswa kujiwekea mpango kazi wa ufugaji
16 December 2024, 8:51 am
Na Adelphina Kutika
Wafugaji wa Kijiji cha Ng’osi kata ya Uhambingeto wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameshauriwa kuweka mipango kazi katika shughuli zao za ufugaji ili kufanya ufugaji wenye tija.
Hayo yamesemwa na Afisa Mifugo kata ya Uhambingeto Alex Sangijo wakati akitoa taarifa yake mbele ya shirika lisilo la kiserikali la Farm for the Future linalotekeleza mradi wa kuwawezesha baadhi ya wananchi katika kijiji hicho mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
Mwanzilishi na mwenyekiti wa Farm For the Future Osmund Ueland amewapongeza wafugaji hao kwa kuwa na viongozi wazuri ambao huwasimamia vyema katika kuendeleza mradi huo utakaowasaidia kuwaingizia kipato
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameshukuru mradi kuingia katika kijiji chao na wamefanikiwa kuzalisha mbuzi wengi ambao huuza maziwa na kuwasaidia katika mbolea wakati wa kilimo.
MWISHO