Nuru FM

Mchungaji aliyedai akifa atafufuka mwili wake wakutwa umeoza

5 December 2024, 8:55 am

Miongoni mwa wananchi wa Kijiji cha Isakalilo akizungumza kuhusu tukio la mchungaji kufariki miezi miwili iliyopita na kutozikwa kwa madai ya kufufuka. Picha na Godfrey Mengele

Na Godfrey Mengele

Hali ya kustaajabisha imetokea katika kijiji cha Isakalilo kilichopo kata ya Kalenga mkoani Iringa umekutwa mwili wa Mchungaji wa Kanisa la Huruma Mch John Wilson Chiba aliyefariki dunia tangu mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba 2024 huku kukiwa na taarifa kwamba aliwataka waumini wake asizikwe kwa madai kuwa atafufuka.

Akizungumza na Nuru FM Mwenyekiti wa kijiji cha Isakalilo Gaspel Mpiluka amesema mchungaji huyo alikuwa anaumwa lakini tangu serikali ya kijiji itoe fedha mwezi wa 9 apelekwe hospital yeye hakutaka kwenda hospitali.

Sauti ya Mwenyekiti

Mwenyekiti huyo anasema kuwa alipokea taarifa uwepo wa harufu kali inayotoka katika nyumba hiyo ndipo walipofika kukuta kifo cha Mchungaji huyo huku muumini anayehudumia maiti hiyo akidai kuwa mchungaji wao hajafa na atafufuka.

Sauti ya Mwenyekiti

Mmoja wa majirani na mchungaji huyo anasema nyumba katika eneo hilo zinapatikana mbali hivyo ilikuwa ngumu kutambua kwa kuwa hakuna mwananchi aliyeweza kufika na kugundua kama kuna jambo limetokea.

Sauti ya Jirani

MWISHO