Nuru FM

Iringa kuwapa kipaumbele walemavu, wazee na wajawazito uchaguzi serikali za mitaa

26 November 2024, 1:20 pm

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James akuzungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za Mita 2024. Picha na Ayoub Sanga

Na Zahara Said na Aisha Ibrahim

Kuelekea Uchaguzi wa serikali za Mitaa hapo kesho Nov 27, Serikali Wilaya ya Iringa imeweka utaratibu wa kuwapa kipaumbele wanawake wajawazito, wazee na watu wenye mahitaji Maalumu ili waweze kushiriki katika uchaguzi huo.

Akizungumza na Nuru FM Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Kheri James amesema kuwa makundi hayo hayatakaa katika Foleni huku akiwataka wananchi kuwapa nafasi ya kupiga kura na kutokaa katika foleni wakati wa zoezi hilo.

Sauti ya DC Kheri

Akizungumzia Hali ya Usalama, Mh. Kheri amesema kuwa usalama umekuwepo katika kipindi chote cha kampeni na tayari wameanza kusambaza vifaa vya uchaguzi katika maeneo yote huku akiwasihi wananchi kujitokeza katika uchaguzi huo.

Sauti ya DC

Kwa upande wao baadhi ya wananchi Manispaa ya Iringa wamesema kuwa wanatarajia kupata viongozi watakaosikiliza na kutatua kero zao.

Sauti ya wananchi

Uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27 mwaka huu unaongozwa na kaulimbiu inayosema’Serikali za mitaa,Sauti ya Wananchi,Jitokeze kushiriki uchaguzi”.