Walimu na wanafunzi Mafinga kunufaika na Mradi wa water for Afrika
8 November 2024, 9:48 pm
Na Fredrick Siwale
Wanafunzi na walimu wa shule ya Msingi Mafinga Mkoani Iringa wanatarajia kunufaika na Mradi wa Maji ya kisima kilichochimbwa na shirika la Water for Afrika.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Mafinga Bi.Sifa Gerana,wakati wa mapokezi ya mradi wa kisima cha kilichochimbwa kwa Ufadhili wa Shirika la Water for Afrika na kuongeza kuwa uwepo wa mradi huo utasaidia wanafunzi kuingia darani kwa wakati kwani walikuwa wakitumia muda mrefu kwenda mitaani kuteka maji.
Awali Meneja wa Water for Afrika Tanzania Bw Nestor Sanga amewataka Wadau wa taasisi kuulinda mradi huo kwa maslahi ya kizazi Kijacho.
Mkurugenzi wa Shirika hilo upande wa Tanzania na Australia Bw.Philipo Hepworth,alisema ni vema kusaidia kusaidia wengine bila kuweka maslahi binafsi na kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.Joseph Kasanga alisema anawashukuru Water for Afrika, Serikali na Wadau kwa kuwatua Kidumu Wanafunzi wa Shule hiyo huku mtadi huo pia ukiwanufaisha wananchi wanaozunguka shule hiyo
Akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wenzake Mwanafunzi Jackson Lupenza aliwashukuru Water for Afrika, Wazazi,Walimu na Viongozi wa Serikali kwa kuwaondolea adhana ya kuitwa Wanaosoma Shule za Vidumu.
MWISHO