Nuru FM

Wilaya ya Kilolo mguu sawa kwa uchaguzi serikali za mitaa

17 September 2024, 10:32 am

Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Hassan Juma Mnyikah akizungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa. Picha na Ayoub Sanga.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unahusisha kuchagua viongozi kwenye nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Mchanganyiko) na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake).

Na Hafidh Ally

Kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa hapa Nchini, Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Hassan Juma Mnyikah ametangaza amri ya mgawanyo wa maeneo ya utawala katika Wilaya hiyo.

Mnyikah amesema wilaya ya kilolo ina mamlaka ya mji mdogo ambayo ni ilula,kata 24,vijiji 94 na vitongoji 484 na ndiyo maeneo yatakayo Shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji , vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji wasio  zidi 25 kwa kila kijiji.

Sauti ya Msimamizi uchaguzi

Aidha amewataka viongozi wa Wilaya ya Kilolo kushirikiana katika kuwahamasisha wananchi wao kujiandikisha ili waweze kupiga kura.

Sauti ya Msimamizi wa Uchaguzi

Katika hatua nyingine Hassan ameishukuru serikali kwa kufanya maandalizi makubwa yatakayosaidia wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka na watakaowaletea maendeleo.

Sauti ya Msimamizi wa Uchaguzi

Uchaguzi wa serikali za Mitaa unaenda kufanyika Nov 27 2024 ambapo Kauli mbiu inasema serikali za mitaa, sauti ya wananchi , jitokeze kushiriki uchaguzi.

MWISHO