TCRA wakutana na watoa huduma za utangazaji Iringa
3 May 2024, 9:16 pm
Na Joyce Buganda
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya mkutano na watoa huduma za utangazaji (Redio na Televisheni za Mitandaoni) na huduma za Mawasiliano wenye leseni mkoani Iringa.
Mkutano huo umefanyika May 03, 2024 katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Iringa ukiongozwa na na Meneja wa TCRA kanda ya Nyanda za Juu kusini, Mhandisi Boniface Shoo.
Lengo la mkutano huo ni kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazosimamiwa na TCRA, kufafanua matakwa na masharti ya leseni, viwango vya ubora na huduma za wateja kupitia mifumo ya mamlaka hiyo.
Mkutano huo pia unalenga kuongeza uelewa na ushirikishwaji wa watoa huduma katika kuboresha usimamizi wa sekta unaokidhi mahitaji ya sasa na kupelekea utoaji wa huduma bora na salama za mawasiliano ya kieletroniki na posta zinazowezesha ustawi wa jamii ya Watanzania.