Pambazuko FM Radio

Wakina Baba Shirikini Kliniki Kilombero

12 November 2026, 12:20

Pichani Muuguzi akimpatia Chanjo Mtoto aliyepelekwa Kliniki picha na Mtandao

upokeaji wa Elimu ya Afya ni Jumuishi kwa Baba na Mama hivyo ni Muhimu sana kwa Akina Baba kushiriki Kliniki kwa nia ya kupata elimu hiyo-Afisa Ustawi

Na Henry Mwakifuna

Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Liliani Sadatale, amesema ushiriki wa baba katika kliniki za mama na mtoto una mchango mkubwa katika kuboresha afya na ustawi wa familia.

Akizungumza na Pambazuko FM, amesema baba anapohudhuria kliniki pamoja na mwenzi wake hupata elimu kuhusu afya ya mama mjamzito, lishe bora, dalili za hatari na maandalizi ya kujifungua salama.

Ameongeza kuwa ushiriki huo humwezesha baba kufuatilia afya na ukuaji wa mtoto, huku ukiimarisha ushirikiano wa wazazi katika kufanya maamuzi na kutimiza majukumu ya familia.

mahojiano na Afisa Ustawi