Pambazuko FM Radio

Ujangili unakuingiza kwenye makosa ya jinai-Kipindi

2 May 2024, 7:23 pm

Jamii katika Bonde la Kilombero imetakiwa kufuata sheria zilizowekwa katika kuvuna rasilimali mbalimbali badala ya kufanya ujangili hali ambayo watajikuta wakiangukia kwenye makosa ya jinai.

Mhifadhi Pori la Akiba Kilombero Kamanda Bigilamungu Kagoma amesema ili mtu aweze kuvuna rasilimali zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, uvunaji unaofanyika ni kupitia uwindaji wa kitalii ambao ni kupitia kampuni ya kitalii iliyosajiliwa, na kampuni imiliki kitalu ndani ya eneo la pori na mwindaji anatakiwa kupata leseni ya aina ya wanyama anaohitaji kuwinda.