Pambazuko FM Radio

Sheria: Mwanamke kupata talaka kisheria inawezekana bila mamlaka za dini

17 June 2023, 12:39 pm

Wanancnchi wakimsikiliza msaidizi wa kisheria kutoka Morogoro Chediele Senzighe katika moja ya mikutano katika kata ya Mkula – Ifakara Kilombero – Picha Isidory Mtunda.

Wanawake wengi wametengana kutokana na sheria za dini zao zinazoeleza kuwa hakuna kuachana mpaka kifo kitakapowatenganisha, jambo ambalo limekuwa ni mzigo kwa wanandoa wengi pindi wanapotaka kuachana.

Na; Isidory Mtunda

Mwanamke kupata talaka kwa kufuata sheria inawezekana , badala ya kusubiri kanisa liwatenganishe kitu ambacho kimekuwa kikiwatesa wanawake wengi.

Hayo yameelezwa na wakazi wa kijiji cha Msufini, kata ya Mkula tarafa ya Mang’ula, halmashauri ya mji wa Ifakara, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, baada ya kupata mafunzo ya sheria ya Ndoa, Mirathi na Ardhi ambayo yamekuwa yakitolewa maeneo mbalimbali katika halmashauri ya mji wa Ifakara, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

wananchi wa kijiji cha Msufini, na mwezeshaji MC Chedieli wakifanya zoezi kuhusu suala la mirathi – picha na; Isidory Mtunda

Baadhi ya wakazi hao akiwemo Helena Njalambaya na Erika Samweli wamesema wanawake wengi wametengana kutokana na sheria za dini zao zinazoeleza kuwa hakuna kuachana mpaka kifo kitakapowatenganisha, jambo ambalo limekuwa ni mzigo kwa wanandoa wengi pindi wanapotaka kuachana.                               

sauti za wananchi, Helena na Erica

Chedieli Senzighe msaidizi wa kisheria kutoka Morogoro Paralegal pamoja na  kuainisha aina za ndoa pia amebainisha kuwa talaka ni waraka wa kisheria unaotolewa na mahakama pekee kuthibitisha kuwa wanandoa fulani si wanandoa tena.    

Mwezeshaji Chediele Senzighe kutoka Morogoro Paralegal – picha na Isidory Mtunda

sauti ya Chedieli Senzighe Paralegal – Morogoro

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Msufini, bwana Nikodem Mwalongo, amekiri kuwa mashauri mengi wanayopokea katika ofisi yao  kijijini hapo yaanahusu migogoro ya ndoa hasa baada ya mume kufariki.

sauti ya mwenyekiti – Nikodem Mwalongo

Kituo cha msaada wa kisheria Morogro kinatoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya haki kwa wanawake juu ya sheria ya Ndoa, Mirathi na Ardhi kwa ufadhili wa shirika la The Aga Khan Foundation.