Pambazuko FM Radio

Jamii yahimizwa kupima kifua kikuu

26 March 2024, 1:58 pm

Na Jackline Raphaely

Jamii imekuwa na mwitikio mdogo katika  upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu, hali inayoonyesha kuwa bado kuna changamoto  kubwa ya kuwafikia watu wenye dalili za ugonjwa huo.

Akizungumza katika maadhimisho ya  kifua kikuu Machi 24,2024 yaliyoandaliwa na hospitali ya rufaa ya mtakatifu Fransisko kwa kushirikiana na Mganga Mkuu halmashauri ya  mji Ifakara Pamoja na wadau wa Afya USAID AFYA YANGU KANDA YA KUSINI  dakta Ben Simon Bilali ambaye ni mshauri wa Huduma ya kifua kikuu Mkoa wa Morogoro kutoka USAID AFYA YANGU amesema ili kukabiliana na  changamoto hizo wataalam wa afya wa kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu wanahakikisha kufika mwaka 2030 wanautokomeza kabisa kwa kutoa elimu na matibabu bure.

Sauti ya Dkt Bilali

Dakta Farida Ban ni mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu kutoka Hospital ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisko anathibitisha kuwa elimu inatolewa sana kwa jamii isipokuwa watu wamekuwa  na madai kwamba ukipima kifua kikuu lazima upime na ukimwi, jambo ambalo linawatia hofu kufahamu ikiwa ameambukizwa virusi vya ukimwi na si kuwa na kifua kikuu ,hivyo amewaomba wananchi kuachana na dhana hivyo badala yake wajitokeze kupima ambapo pia ametaja dalili za ugonjwahuo.

Sauti ya Dkt Farida Ban

Maadhimisho hayo ya kifua kikuu yamefanyika katika viwanja vya ukumbi wa Vijana wa Mt. Yohane Paulo II Parokia ya  Ifakara na kuhudhuriwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali Wilaya ya Kilombero ambapo pia wametoa shukrani zao kwa uongozi wa Hospital ya mtakatifu Fransisko Pamoja na serikali.

Sauti za wananchi

Maadhimisho ya kifua kikuu duniani hufanyika kila mwaka tarehe 24 mweziwa 3 na kwa mwaka 2024  yamebebwa na kauli mbiu isemayo NDIYO  kwa PAMOJA TUNAAWEZA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU