Pambazuko FM Radio

Kituo cha kupooza umeme Ifakara chawashwa, wilaya tatu kunufaika

5 December 2023, 12:49 pm

Wilaya tatu za mkoa wa Morogoro zimenufaika na umeme wa vijijini- REA, baada ya kituo cha kupozea umeme kilichopo Ifakara kata ya Kibaoni kuwashwa na kuanza kazi.

Na; Isidory Mtunda

Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro kunufaika na Umeme wa REA, baada ya kituo cha kupozea Umeme kuwashwa rasmi Desemba tatu mjini Ifakara katika kata ya Kibaoni.

Akizungumza wakati wa Uwashaji wa umeme katia kituo cha kupozean umeme{Substationi} katika kata ya Kibaoni  Mjini Ifakra, meneja msimamiza wa mradio wa umeme vijijini {REA}, mhandisi Romanus Rwena, amesema  ujenzi wa kituo hicho kimegharimu  shilingi bilioni 25,huku Bilioni 18 zimetolewa na wahisani ambao ni Umoja wa Ulaya{EU}na Seriali ya Tanzania ikichangia bilioni 7.

Mhandisi Lwena wa mbele akitoa ufafanuzi juu kituo cha kupozea umeme – Picha Isidory Mtunda

sauti ya mhandisi Lwena

Kaimu mkurugenzi wa REA Tanzania Mhandisi Jones Olotu amesema kuwashwa kwa umeme katika kituo hicho  kunaondoa changamoto ya umeme kuwa mdogo kwa wawekezaji ambao walishindwa kuwekeza kutokana na changamoto hiyo.

sauti ya Mhandisi Olotu

Naye mkuu wa wilaya Kilombero, Wakili Danstan Kyobya amewashukuru wafadhili wa mradi huo kwani mradi utaleta maendeleo na kufungua milango ya uwekezaji kwa halmashauri ambazo zitanufaika na mradi huo.

Wataalam, viongozi na wananchi wakimsikiliza DC Kyobya ( aliyenyoosha mkono_ picha na I. Mtunda

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kilombero, wakili Danstan Kyobya

Viongozi wa chama & serikali, wataalamu wa Umeme na wananchi – Picha na Isidory Mtunda

Nao baadhi ya viongozi serikali kata ya kibaoni, Aziza Salumu Kilimo Hwaya wamesema umeme huo utaongeza fursa hasa katika mashine za kukoboa mpunga na kuongeza kipato kwa jamii.

Sauti za wananchi