Pambazuko FM Radio

Aliyesombwa na mafuriko mwili wake umepatikana

26 March 2024, 4:11 pm

Wananchi wakiwa kwenye msiba wa Kijana aliyefariki kwa kusombwa na mafurioko{Picha na Elias Maganga}

Na Elias Maganga

Mwili wa Kijana Shafii Abas Kambeyu aliyesombwa na mafuriko wakati akiwa anawavusha watu wengine katika daraja la Katindiuka halmashauri ya Mji wa Ifakara umepatikana.

Akizungumza na pambazukofm Mwenyekiti wa Mtaa wa Katindiuka A Mulla Mlamba amesema mwili wa kijana huyo umepatikana march 25 mwaka huu majira ya saa moja jioni.

Bwana Mlamba amesema baada ya jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vingine kuutafuta mwili huo kuanzia asubuhi   hadi mchana hawakufanikiwa kuupata,ilipofika saa kumi jioni vijana waliendelea na zoezi la kuutafuta na kufanikiwa kuupata saa moja jioni.

Sauti ya mwenyekiti wa Mtaa wa Katindiuka A Bwana Mulla Mlamba

Baba mzazi wa  marehem Bwana Abas Kambeyu amesikitishwa na kifo cha mwanae na ametoa wito  kwa jamii kuwa makini hususan katika kipindi hiki cha mvua za masika

Picha ya bwana Abas Kambeyu baba mzazi wa marehemi{Picha na Elias Maganga]
Sauti ya Bwana Abas Kambeyu

Viongozi mbalimbali akiwemo katibu tawala wa Wilaya ya Kilombero Bwana Abraham Mwaikwila ni miongoni mwa waliofika msibani kuwafariji wafiwa na waombolezaji  ambapo amesema  marehemu alikuwa na nia njema ya kuwaokoa wengine, na amewapongeza vijana waliofanikisha kupatikana kwa mwili wa marehemu.

Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Abraham Mwaikwila {Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero Abraham Mwaikwila

Kwa upande wao Vijana wa Katindiuka wamesikitishwa kumpoteza kijana mwenzao ambaye alikuwa mpambanaji, anajituma katika shughuli za utafutaji.

Picha ya Kijana wa Katindiuka
Sauti za baadhi ya Vijana wa Mtaa wa Katindiuka wakielezea masikitiko yao kutokana na kifo cha kijana mwenzao

Mazishi ya Kijana huyo Shafii yamefanyika march 26 mwaka huu majira ya saa saba mchana huko huko  Katindiuka.