Pambazuko FM Radio

Wananchi Watakiwa Kuchangia Maendeleo ya Shule

25 June 2021, 5:51 am

Na:Katalina Liombechi

Wananchi wa Kata ya Igawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wameombwa wawe na Utaratibu wa kuchangia michango ya Shule  bila kujali kuwa ana au hana Mtoto anayesoma katika shule husika.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Igawa bwana SEVELUSI AMAN KAMGUNA Wakati anazungumza na Pambazuko Fm ilipotaka kujua juu ya miradi ya shule hususan  katika upande wa Elimu.

Diwani KAMGUNA amebainisha njia bora ya Kuanzisha vyanzo vya Mapato katika Kata ni Kushirikisha Jamii na Wadau mbalimbali wa Elimu  ili kupata Mawazo na Maoni juu ya uanzishwaji wa Vyanzo hivyo  huku akitaja chanzo Kikuu cha Mapato kwa sasa katika Shule zake ni Kilimo.   

Diwani KAMGUNA

Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Masuala ya Elimu na Mazingira la  Save Education and Future Development foundation  Bwana Clarensi Mosha amesema Shirika hilo liko  tayari kushirikiana uongozi wa kata hiyo ili  kuwapatia mawazo ya kubuni vyanzo vya Mapato yakayowezesha  kukuza Elimu katika Kata hiyo

Neema Taita na Tasibu Abeid  ni Miongoni mwa Wananchi waishio katika Kata hiyo wamesema wapo tayari kuchangia endapo utaratibu wa Uchangiaji utawekwa wazi.