Pambazuko FM Radio

Morogoro: Wananchi kijiji Minepa wailalamikia serikali ya kijiji kuwapora mashamba

17 June 2023, 1:46 pm

Mafunzo yaliyotolewa na Morogro Paralegal, juu ya sheria ya  ndoa, talaka, mirathi na ardhi, yameibua mashauri mbalimbali kwa wananchi wa kata ya Minepa, wilaya ya Ulanga,  ambao walihudhuria mkutano huo.

Na; Isidory Mtunda

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Minepa, kata ya Minepa, wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, wameilaumu serikali ya kijiji hicho kwa kitendo cha kupora mashamba yao na kuwakodishia watu wengine.

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo juu ya sheria ya Ardhi, Ndoa, Talaka na Mirathi yaliyoendeshwa na kituo cha msaada wa kisheria Morogoro, ambapo Hidaya Mgalakachua na Rashidi Lihoki wamedai kuwa serikali ya kijiji hicho imepora mashamba yao na kusababisha  maisha yao kuwa magumu kwani wanategemea kilimo ili kutunza familia zao.

mwenye microphone ni Hidaya Mgalakachua – picha na; Isidory Mtunda

Akifafanua juu ya malalamiko ya wananchi hao mwenyekiti wa kitongoji cha Kisakimbali, kata ya Minepa, wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, Fadhili Mhawi, amesema wananchi hao walipewa maeneo hayo kama msaada kwa kuwa walikuwa wageni na hawakuwa na mahali pa kulima.

Mwenyekiti wa kitongoji – Fadhili Mhawi – picha na Isidory Mtunda

Sauti ya Fadhili Mhawi

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Minepa , kata ya Minepa, tarafa ya Lupiro, wilaya ya Ulanga, mkoa wa Morogro Nasoro Nyomela amesema eneo lile ni la kijiji na maamuzi yaliyofanyika ni ya wanakijiji wote, na ameshauri kuwa kama wanahisi wamedhulumiwa wanaweza kwenda ngazi za juu kwa msaada zaidi.

picha ya mwenyekiti wa kijiji Nasoro Nyomela – picha na; Isidory Mtunda

sauti ya Nasoro Nyomela

Joyce Peter ni mwanasheria kutoka kituo cha Morogoro Paralegal, amesema mikutano hiyo inafanyika kwa lengo kuwawezesha wanawake kiuchumi na kutambua haki zao, chini ya mradi wa POWER, kwa ufadhili wa The Aga Khan Foundation.

Picha ya Joyce Peter mwanasheria kutoka Morogoro Paralegal Center – picha na’

Sauti ya mwanasheria Joyce Peter