Pambazuko FM Radio

Wananchi Wachangia Ujenzi wa Madarasa

18 May 2021, 5:50 am

Wananchi wa Mtaa wa Jongo,Kata ya viwanja sitini  katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero wamechanga  mchango  wa fedha kiasi cha shilingi milioni tatu  na Elfu tisini kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maadarasa katika shule ya sekondari ya kwa shungu.

Mwananchi Grec Mdaila

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Emanuel Lusoli  amesema kuwa mchango huo umeanza kuchangwa tangu mwezi  desember mwaka jana ambapo kila mwananchi ambae ni nguvukazi anachangia shilingi elfu mbili,  na mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha.

Bwana Lusoli amesema licha ya kukusanya kiasi hicho cha fedha bado baadhi ya wananchi hawajachangia kutokana na sababu mbalimbali na hivyo ikawalazimu zoezi hilo la kuchangisha fedha kulisogeza mbele huku mkutano mkubwa ukitarajiwa kufanyika mwezi june ili kujua mwisho wa mchango huo.