Pambazuko FM Radio

Jamii yatakiwa kuchukua hatua kukabiliana na Uharibifu wa Bionuai-Kilombero

2 May 2024, 7:17 pm

Matumizi ya Nishati Mbadala na Majiko Banifu vimetajwa kusaidia Kupunguza utegemezi wa Mazao ya Misitu na kuelezwa kuwa njia moja wapo ya kukabiliana na Uharibifu wa Bianoai.

Isack Shonga ni Afisa Mazingira Kutoka Shirika la Association Maingira ameyasema hayo wakati akizungumza na Pambazuko fm juu ya Namna ya kukabiliana na uharibifu wa Bionuai unaotokana na Matumizi ya Nishati ya Kupikia.

Amesema Matumizi ya Mkaa mbadala na Majiko banifu ni gharama nafuu kiasi ambacho mtu yeyote anaweza kumudu.